WAZAZI WATAKIWA KUFUATILIA MAUDHURIO YA
WATOTO WAO WAKIWA SHULE.
WATOTO WAO WAKIWA SHULE.
.
Wazazi wilayani Njombe mkoani Iringa wametakiwa
kufuatilia mahudhurio ya watoto wao mashuleni ili kuweza
kujua maendeleo yao kiundani katika kuboresha kiwango cha elimu wilayani hapa.
Hayo yamebainishwa na mkaguzi mkuu wa shule za msingi wilayani Njombe BI.SARAH CHIWANGU ambaye amepewa dhamana ya kukagua shule mbalimbali katika kipindi hiki cha mitihani ya kidato cha pili akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.,BI.CHIWANGU ameeleza kuwa halmashauri ya wilaya ya njombe ina jumla ya shule 53 zenye wanafunzi wa kidato cha pili wanaoendelea kufanya mtihani huo,ambapo halmashauri ya mji ina jumla ya shule 19,na halmashauri ya wilaya ina jumla ya shule 34 ambazo zinakamilisha idadi hiyo.
Aidha,ameyataja baadhi ya matatizo ambayo yamewapelekea baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanya mitihani hiyo, kuwa ni pamoja na utoro ugonjwa na maradhi mbalimbali hali inayoweza kupelekea kushuka kwa kiwango cha taaluma wilayani hapa.
Katika hatua nyingine amewataka wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wanatarajia kufanya mtihani huo mwakani kujua umuhimu wa kufanya mitihani ya kidato cha pili kwani ndio inayowapa nafasi ya kuja kufanya mtihani wa kidato cha nne hivyo wasijisahau kwa vile hakuna mchujo wa kuingia kidato cha tatu.
No comments:
Post a Comment