Monday, November 22, 2010

MBOLEA ZA RUZUKU MKOANI NJOMBE

MBOLEA ZA RUZUKU MKOANI NJOMBE ZAPUNGUZA MACHUNGU KWA
WANANCHI WILAYANI HUMO.


Wananchi wilayani Njombe Mkoani Iringa wamefurahishwa na kitendo cha utaratibu waserikali kubandika majina yao mapema juu ya watakao nufaika na mbolea za ruzuku ili kuondoa usumbufu wa kupanga foleni bila kujua kama watapata vocha.

Waandaaji wa safu hizi wamefanikiwa kufika katika Ofisi ya Serikali ya mtaa wa kibena kati na kuwakuta wananchi wakitazama majina yao.katika maoni yao wamevishukuru vyombo vya habari kwa kutangaza ubadhilifu uliotokea mwaka jana katika ugawaji pembejeo hizo na kudai kuwa vimepeleka kuweka utaratibu.

Aidha Afisa Mtendaji wa mtaa huo bwana OTMAR DANIEL MBANGALA ametoa maelekezo ya upokeaji vocha hizo kuwa ni lazima kujaza fomu ya mnufaika wa pembejeo hizo na kwamba yeyote ambaye hataridhika na mfumo huo anatkiwa kuwasilisha malalamiko yake kwenye balaza la kijiji.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi hao kutoleta vurugu pindi vocha hizo zitakapo anza kutolewa kwani watakao simamia mchakato huo hawatanufaika na pembejeo hizo kwani watafanya kazi hiyo kwa kujitolea bila malipo hivyo amewataka kujua kuwa kwa mtaa huo wamepata vocha 1150 na kuwepo na upungufu wa vocha 1339.

Akijibu swali la wananchi waliouliza juu ya mabadiliko ya bei za pembejeo hizo kwa karibu kila mwaka,Bwana kindamba ambaye ni wakali wa pembejeo hizo katika mtaa wa kibena kati amewataka kujua kuwa mamlaka ya kubadili bei hizo ni mamlaka ya wahisani wenyewe wanaoleta pembejeo hizo.

No comments:

Post a Comment