Tuesday, November 16, 2010

TATIZO LA MAJI MKOA WA IRINGA

TATIZO LA MAJI MKOA WA IRINGA
KIJIJI CHA MIGOLI.


Wananchi wa Kijiji cha Migoli Mkoani Iringa wameelezea adha kubwa ya maji wanayoipata kwa kipindi cha miezi sita sasa kutokana na kuharibika kwa mtambo wa kusukumia maji kijijini hapo.

Wananchi hao Wamesema Awali walikuwa wakipata huduma hiyo ya maji kutoka kijiji cha Izazi kilichopo kilomita kumi kutoka Iringa lakini kwa kipindi cha miezi sita sasa tangu kuharibika kwa mtambo huo hali ya maisha imekuwa ngumu kwao kutoka na tatizo hilo la maji kwa maeneo mengi ya kijiji hicho.

Kutokana na hali hio imewalazimu wananchi hao kutumia maji kutoka Bwawa la Mtera na visima vya kuchimba kwa mkono ambapo imeelezwa kuwa maji wanayokuwa wanayapata kutoka katika vyanzo hivyo yametajwa kutokuwa Salama kwa matumizi ya Binadamu na kuwapelekea kuwasababishia magonjwa ya kuahara na kichocho miongoni mwao wakiwa watoto wadogo katika kijiji hicho.

Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Iringa Bw Lukas Madaha Amesema Tayari Idara yake imeanza hatua za Awali katika kulitatua Tatizo hilo linalowakabili wakazi hao wa kijiji hicho cha Migoli mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment