KUBADILIKA KWA MITAALA YA ELIMU MARA KWA MARA KUNAONGEZA KUSHUKA KWA ELIMU NJOMBE.
Tabia ya Serikali ya kubadilishabadilisha Mitaala mara kwa mara katika Shule za Msingi na Sekondari imeelezewa kuwa Sababu Mojawapo inayochangia kuporomoka Kwa Kiwango cha Elimu Wilayani Njombe
Hatua Hio pia imesababisha kuendelea kwa Tatizo la Upungufu wa Vitabu katika Shule za Msingi kwani Shule hulazimika kununua Vitabu Vipya kila Mtaala unapobadilika hali ambayo shule nyingi hazina Uwezo huo
Wakizungumza na mtandao huu katika Maadhimisho ya Wiki ya Vitabu Nchini katika Maktaba ya Wilaya ya Njombe Baadhi ya Wadau wa Elimu Wamesema Kila Wakati Serikali inapobadilisha Mitaala husababisha kuongezeka kwa Tatizo la Vitabu kwani Vile vilivyonunuliwa Awali Havitumiki Tena katika mitaala hiyo mipya.
Wamesema Tatizo Nyinyine linalosababisha kuendelea kwa Tatizo la Vitabu kwenye Shule za Msingi ni upungufu wa Fedha ya Ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia Mradi wa MMEM ambao haukidhi mahitaji ya Shule zote
Kwa Mujibu wa Takwimu za Wilaya ya Njombe Yenye Jumla ya Shule 181 ni Shule sita Tu Ndio Zenye Maktaba ambazo pia Zinakabiliwa na Upungufu wa Vitabu
Takwimu hizo za Hali ya Upatikanaji Vitabu katika Shule Hizo zinaonesha kuwa kutokana na Idadi ya Wanafunzi Sabini na Sita Elfu,Mia Tatu Sitini na Sita wanafunzi Watatu hulazimika kuchangia Kitabu Kimoja kitu kinachopelekea kurudishwa nyuma kitaaluma.
No comments:
Post a Comment