MIAKA MITATU YA UPLANDS FM RADIO(NJOMBE).
Tamasha la kutimiza kwa miaka mitatu ya Radio Uplands Fm katika mkoa wa Njombe walayai hapa linafanyika leo katika viwanja vya saba saba mchana baadae kufuatia na shoo ya muziki katika ukumbi wa Vegas uliopo mjini hapa.
Akiongea na mtandao huu kwa kwa nyakati tofauti Meneja wa radio hiyo ya Uplands Fm bwana Vitus Swale amesema kuwa tamasha hilo litaanza mnamo saa tatu asubuhi,ambapo kutakuwa na michezo mbali mbali katika viwanja hivyo vya saba saba.
Amesema kuwa baadhi ya mambo yatakayokuwepo uwanjani hapo ni pamoja na mchezo wa mpira wa miguu,ambao utawakutanisha timu ya mpira wa miguu ya Uplands Fm na Chuo cha ualimu Hagafiro kilichopo wilayani njombe.
Pia ameongeza kuwa mbali na mchezo wa kandanda pia kutakuwa na mchezo wa mpira wa pete kwa wasichana,mpira wa wavu,kukimbia na hata kuvuta kamba.
Mbali na mashindano hayo pia kutakuwa na bendi na vikundi mbali mbali vya muziki ambapo vijana wa kizazi kipya kutoka wilayani hapa wataongozwa na mwanamuziki kutoka jijini dar es salaam BELLE 9 anayetamba na nyimbo zake za MASOGANGE,WE NI WANGU NA LADHA YA MAPENZI.
Katika kuadhimisha miaka hiyo mitatu kituo hicho cha radio cha Uplands Fm kitasoma risala yake toka kuanzishwa kwake hadi kufanikiwa kutimiza miaka mitatu leo siku ya tarehe 28 mwezi huu wa kumi na moja,mbali na risala hiyo itakayosomwa mbele ya mgeni rasmi katika shughuli hiyo mkuu wa wilaya ya Njombe Bi. SARA DUMBA pia zitasomwa risala za wadau wa radio kutoka sehemu mbali mbali.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya wakazi wa wilaya ya Njombe wamesema kuwa toka kuanzishwa kwa radio ya Upland mkoani hapa Njombe,imewasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuwahabarisha na hata kuwaburudisha kwa vipindi mbali mbali vya habari na burudani vinavyorushwa na kituo hicho cha radio mkoani hapa.
Na miongoni mwa watangazi na waandishi wa kituo hicho ni pamoja na ASIFIWE NGAO(MSIMAMIZI WA VIPINDI),SHABANI LUPA(MHARIRI MKUU),FESTUS PANGANI,(MTANGAZAJI,MWANDISHI),HAMISI KASAPA(MTANGAZAJI MWANDISHI),BENNY NGINDO (MTANGAZI,PRODUCER),SARA MANDE(MTANGAZAJI),CONSOLATA KIOMBO(MTANGAZAJI),GABRIEL KILAMLYA(MWANDISHI),SHEDRACK MWANSASU(MTANGAZAJI)BRAISON MGOJI(MTANGAZAJI),DAVID JOTHAM(MTANGAZAJI).
Sherehe hizo za kutimiza miaka mitatu zitafanyika katika viwanja vya saba saba wilayani njombe.
No comments:
Post a Comment