WANANCHI WILAYANI NJOMBE MKOANI IRINGA WAMETAKIWA KULIPA KODI ZA MAJENGO YAO.
Wananchi Wilayani Njombe Mkoani Iringa wametakiwa kulipa kodi ya majengo ya nyumba zao kabla ya mabadiliko ya bei mpya itakayoanza mapema ifikapo Januari 2011kutokana uthaminishaji mpya wa majengo kutoka wizara ya ardhi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa mtaa wa NAZARETH bwana COMRED JOHN .J.MTITU akizungumza na na mwandishi wa habari hii ofisini kwake juu ya mabadiliko ya bei mpya za kodi za ardhi.
Bwana MTITU amesema kuwa wananchi wa wamaeneo yake kama NAZARETH wanatakiwa kufika katika ofisi ya Melinze na wengine kufika kwenye shule mpya inayoendelea kujengwa Nazareth ilikupewa bei halisi ya nyumba ya kila mmoja ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko hayo.
Akitolea mfano wa ongezeko la bei ya nyumba moja ya bwana TEUDOLI MLOWE mkazi wa NAZARETH, mwenyekiti huyo amesema,bei ambayo inafahamika ni shilingi Elfu tatu lakini bei mpya iliyofika kwenye nyumba ya bwana huyo mpaka sasa ni zaidi ya shilingi elfu ishirini na nne.
Aidha ameongeza kuwa,kwa wale wote walioomba kupimiwa viwanja vyao wanatakiwa kufika kulipia fedha kwaajiri ya zoezi hilo kwani MKURABITA wanaohusika na suala hilo watafanya kazi hiyo mpaka November 30 mwaka huu tu hivyo atakayepuuzia zoezi hilo hataweza kusaidiwa.
No comments:
Post a Comment