WATENDAJI KATIKA SEKTA YA AFYA MKOANI IRINGA WASHAURIWA KUBORESHA HUDUMA.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dokta Ezekiel Mpuya Amewaelekeza Watendaji wa Afya katika Halmashauri za Manispaa Mkoani Humo kubadili Mtazamo wao katika kufanyamaamuzi ya Rasilimali Watu kwa Lengo la Kuboresha Utolewaji wa huduma za Afya kwa Wananchi
Dokta Mpuya alikuwa akizngumza na Watendaji hao wa Afya Waliokutana Mjini Iringa Katika mafunzo ya Menejimeni ya Rasilimali Watu yaliokusudia Kuboresha Huduma za Afya Mkoani Iringa.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Mganga huyo Amesema sekta ya Afya Mkoani Iringa ni Moja ya Sekta Zinazokabiliwa na Changamoto Mbalimbali ikiwemo upungufu wa Rasilimali watu hususani Maeneo ya Vijijini hali ambayo husababisha Misongamano ya Watu katika Vituo vya Afya na Zahanati hali ambayo husababisha Malalamiko kutoka kwa Wananchi.
Kwa Upande wao Madaktari wanaoshiriki katika Mafunzo hayo kutoka Wilayani Njombe wamesema Njia pekee kwa Serikali kuboresha Huduma ni kuongeza Vitendea kazi pamoja na kuongeza Motisha kwa Wafanyakazi katika sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment