Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi wilayani kilosa
kutowapokea wafugaji bila mpangilio kwani ndio sababu kubwa ya migogoro ya mara
kwa mara wilayani humo.
Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania Jakaya Kikwete akiwa anaongea na wananchi wa wilayani kilosa mkoani morogoro.
Ameyasema hayo August 24,mwaka
huu katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani kilosa mkoani morogoro
ambapo amekagua mradi wa kufua umeme wa maji kisanga pia ameweka jiwe la msingi
katika barabara ya kiwango cha lami kutoka Dumila hadi Rudewa.
Aidha Kikwete amesema kuwa
viongozi wasiwe wakarimu kupita kiasi cha kuwakalibisha wafugaji wengi katika
eneo moja na kusema kuwa mifugo inaongezeka lakini ardhi haiongezeki pia
amezungumzia swala la wahanga wa mafuriko wa 2010 kuhusu kupatiwa viwanja kwa
ajili ya makazi mapya ambapo amemhoji mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
kilosa kuhusu swala hilo na mkurugenzi kuahidi kuanza kulishughulikia zoezi
hilo la ugawaji wa viwanja mwanzoni mwa wiki hii.
Wananchi waliokusanyika kwa ajili ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr,Jakaya Kikwete
Sambamba na hayo Rais kikwete
amekumbana na changamoto nyingi za wananchi wa wilayani kilosa ambapo wananchi
wa wilayani kilosa wanauhitaji wa maji safi na salama,barabara ya lami pamoja
na umeme mambo ambayo ameyasema kuwa yapo kwenye mchakato.
Wakwanza kutoka kulia ni MKuu wa mkoa wa Morogoro John Bendera na wa kwanza kutoka kushoto ni mbunge wa jimbo la mikumi Sas ges.
Katika ziara hiyo ya Rais kikwete
pia ameambatana na waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli ambaye naye ameongea na
wananchi wa kilosa kuhusu ujenzi wa barabara ya lami itokayo Dumila hadi mikumi
na kusema kuwa ujenzi huo wameugawa kwa awamu tatu awamu ya kwanza ni kutoka
Dumila hadi Rudewa ambapo ujenzi huo tayari umeshakamilika na awamu ya pili ni
kutoka Rudewa hadi kilosa na mwisho kutoka kilosa hadi mikumi.
Mheshimiwa Jakaya kikwete akihojiana na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilosa
Aidha mbunge wa jimbo la kilosa
Mustafa Mkulo amemuuomba Rais kikwete kukamilisha ujenzi huo wa barabara ya
lami kwabla hajaondoka madarakani kwa ajili ya kuwapatia maendeleo wakazi wa
wilayani kilosa.
Wananchi wakitawanyika mara baada ya mkutano
Pia Rais kikwete amezawadiwa
zawadi mbalimbali kutoka wilayani kilosa ikiwa ni pamoja na ng’ombe wawili
majike na wote wanamimba na dume moja la ng’ombe,kinyago cha tembo kutoka
TANAPA picha ambayo wamemchora Rais kikwete pamoja na mchele tani moja ambao
unalimwa wilayani kilosa mkoani morogoro.