Monday, August 25, 2014

MAHAFARI YA 39 YA SHULE YA MSINGI MAZINYUNGU YAFANA YASABABISHA KUTATUA KERO ZA SHULENI HAPO.

Shule ya msingi mazinyungu inakabiliwa na changamoto ya kukosa uzio wa shule hali inayopelekea wasiwasi mkubwa wa amani kutokana na shule hiyo kuwa na kitengo maalum cha watoto walemavu wasioona na walemavu wa ngozi [Albinism].
                                         Meneja wa NMB tawi la kilosa Lameck Matemba
Hayo yamebainishwa august 22 mwaka huu kwenye mahafari ya 39 ya wahitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi mazinyungu ambapo kwa mwaka 2014 huu wanahitimu wanafunzi 88 wasichana wakiwa 45 na wavulana 43 na wanaotarajiwa kuhitimu darasa la saba kati ya hao walemavu ni sita wakiwemo wasichana watano na mvulana mmoja,ambapo katika risala hiyo iliyoandaliwa na shuleni hiyo imeeleza kuwa hali wa wanadamu kwa sasa imebadilika kutokana na baadhi ya watu wasio wema kuwasaka walemavu hao wa ngozi kwa imani za kishirikina kwa kueleza kuwa shuleni hapo waendesha pikipiki hupita mara kwa mara na wakiwa mwendo wa kasi hali ambayo ni hatari kwa wale walemavu wa macho.
                Meneja wa Benk ya NMB Lameck Matemba wa pili kutoka kulia akifuatiwa na mwalimu mkuu wa shule ya mazinyungun Lameck Mkude ambaye niwatatu kutoka kushoto


Sambamba na hayo shule hiyo ya mazinyungu inakabiliwa na changamoto ya ukosefu madawati hali inayopelekea wanafunzi kukaa wengi katika dawati moja na kueleza kuwa pamoja na upungufu wa madawati shuleni hapo wanauhitaji mkubwa wa SIMTANK kwa ajili ya kuhifadhia maji shuleni hapo.Pia serikali imeombwa kuwajali walimu ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara kwani inadidimiza kiwango cha ufaulu mashuleni.
                      Wanafunzi wahitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi mazinyungu iliyopo wilayani kilosa mkoani Morogoro
Katika mahafari hayo yaliyohudhuliwa na Meneja wa Bank ya NMB tawi la kilosa ambaye ndiye aliyekuwa mgeni Rasmi Lameck Matemba amesema kuwa kuhusu changamoto zilizotajwa shuleni hapo wao kama Benk ya NMB wapo tayali kuisaidia shule hiyo na kwani tayari wameshaandika andiko kwenda makao makuu kuhusu changamoto mbalimbali za shuleni hapo pamoja na hapo meneja huyo ametoa kiasi cha shilingi laki moja na nusu kwa ajili ya chakula kwa wale wahitimu wa darasa la saba siku ya mtihani.
                    Watoto wenye ulemavu ambao ni kitengo maalum katika shule ya msingi mazinyungu
Ameongeza kwa kuiasa jamii kuwa wawe walinzi wazuri kwa watoto wao hasa kwa hawa waliopo shuleni hapo wenye ulemavu kwa kuwajali na kuwapa huduma muhimu na ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa wajipange kwa watoto wao wanaotarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi hivi karibuni na pindi matokeo yanapotoka waweze kujiunga na kidato cha kwanza.
Meneja wa NMB Tawi la kilosa Lameck Matemba akiwapa zawadi walemavu baada ya kuonyesha uhodari wa kupiga ngoma na uwimbaji katika mahafali yao.
Kwa wake Katibu wa chama cha mapinduzi [CCM] wilayani kilosa Dodo Duguli Sambu akizungumza kwa niaba ya wazazi amewapongeza walimu kwa kuwapatia elimu na malezi watoto wao kwa kipindi chote walichokuwa shuleni pia amewaomba wazazi wenzake kuwa na ushirikiano na walimu katika kukuza kiwango cha ufaulu..........cue ya katibu wa ccm kilosa dodo duguli sambu.
Katibu wa CCM wilayani kilosa Dodo duguli sambu akiongea kwa niaba ya wazazi katika mahafari ya 39 ya shule ya msingi mazinyungu.

No comments:

Post a Comment