Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias
Tarimo amewataka viongozi wa vijiji
kutowapokea wafugaji wanaotoka maeneo ya
vijiji vya jirani na kuvamia katika
maeneo ya wakulima.
Baadhi ya mifugo iliyopo kijiji cha ulaya mbuyuni
Ameyasema hayo agost 11 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake kuhusiana na wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima
wilayani kilosa mkoani morogoro na kusema kuwa katika wilaya yake kuna wafugaji
wengi hivyo hahitaji tena wafugaji kutokana na wilaya hiyo kuwa na wafugaji
wengi na kukwamisha shughuli nyingine za kimaendeleo.
mazao aina ya mbaazi yakiwa yameharibiwa na mifugo katika kijiji cha ulaya mbuyuni
Ameongeza kwa kusema kuwa viongozi
waliopo vijijini wanawakaribisha wafugaji hao kwa kupewa rushwa na wanapoona
mambo yanawashinda huchukua hatua ya
kuwafukuza na na kushindwa kutokana na rushwa ambayo wameshaipokea.
Pia amesema kuwa pindi atakapo baini
kuwa kiongozi yeyote amepokea rushwa kwa ajili
ya kumkalibisha mfugaji katika eneo lake basi atakuwa amepoteza sifa ya
kuwa kiongozi.
mifugo aina ya ng'ombe ikiendelea kula mazao aina ya mbaazi
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa
kilosa kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya wakulima na
wafugaji kwa ajili ya kulinda ardhi na pia kuondoa migogoro.
Kwa upande
wake katibu tarafa wa tarafa ya ulaya Raphael Mvurungu amesema kuwa katika kata
yake ni kweli mifugo ipo lakini hajui wafugaji hao wameingia vipi kutokana na
wenyeviti wa viji kuwatetea wafugaji hao kuwa wanawatambua uwepo wao hivyo
kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria wafugaji hao
Mwenyekiti wa kijiji cha ulaya mbuyuni Rashid Mjomba
Naye
mwenyekiti wa kijiji cha ulaya mbuyuni Rashidi Mjomba amesema kuwa katika
kijiji chake kuna wafugaji wamevamia kijiji hicho na hajui wametoka wapi na
hatua za kuwaondoa wafugaji hao zinachukuliwa na ameeleza kuwa kuna changamoto inayowakumba kwa sasa ni kwa
baadhi ya wananchi kudai kuwa endapo wafugaji hao wa jamii ya kimasai
wataondoka uchumi utashuka kijijini hapo kutokana na wafugaji hao kiuwa wateja
wazuri kiatika biashara zao.
No comments:
Post a Comment