Afisa Tarafa wa tarafa ya
Ulaya Raphael Mvulungu amewataka wananchi kuendelea kuchangia ujenzi wa
Maabara tatu katika shule za sekondari.
Afisa tarafa wa tarafa ya ulaya Raphael Mvulungu
Ameyasema hayo August 10
mwaka huu wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu ujenzi wa
maabara kwa shule za sekondari
utakayogharimu kiasi cha fedha cha shilingi milioni 84 ambapo kwa sasa
wameanza kuchangisha fedha hizo kwa
wananchi kiasi cha shilingi 5000 kwa kila mwananchi ambapo katika Tarafa hiyo
kuna nguvu kazi 5000 ambao wanatakiwa
kutoa mchango huo ambapo hilo ni agizo
la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete ambapo amehitaji
kila shule sekondari iwe na
maabara tatu za Sayansi , Bailojia , Kemia na Fizikia na amehitaji maabara hizo
kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Ukwiva Liberath Patrick Ngure
Kwa upande wake mkuu wa
shule ya Sekondari ya Ukwiva Liberath ngure amesema kuwa mpango huo utasaidia kukuza kiwango
cha ufaulu kwa upande wa masomo ya sayansi na kusema kuwa changamoto iliyopo ni
baadhi ya wazazi kushindwa kujua umuhimu wa maabara na aamewaomba wananchi kwa
ujumla kuwa na moyo wa kuendelea kuchangia ili kukamilisha ujenzi wa maabara
hizo.
wanafunzi wa shule ya sekondari ukwiva wakiwa katika jengo lililojengwa na TANAPA Shuleni hapo
wanafunzi wa shule ya sekondari ukwiva wakiwa katika jengo lililojengwa na TANAPA Shuleni hapo
No comments:
Post a Comment