Wananchi wa wilayani kilombero mkoani morogoro watanufaika na
barabara itokayo Ruaha wilayani kilosa hadi Ifakara wilayani kilombero.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika
ujenzi wa daraja la mto kilombero.
Pia rais kikwete amezungumzia shabaha ya serkali kuwa na
viwanda kumi vya sukari na kusema kuwa mchakato unafanyika ili kupata hekta
laki mbili na nusu kwa ajili ya uwekezaji huo.
Wakati huohuo Rais Kikwete amefungua mradi wa umeme katika
mji wa mwaya unaofadhiliwa na REA ambapo tayari zaidi ya vijiji ishirini na
saba 27 vinanufaika na mradi huo sambamba na kujionea mfumo mpya wa matibabu
ujulikanao kwa jina la TELMEDICINE katika kituo cha afya cha mwaya mfumo huo
unasaidia kutoa matibabu kwa wataalam ambao watakuwa katika kituo kingine kwa
kumpatia mtaalam anayetoa matibabu maelekezo ya nini afanye kwa mgonjwa hasa
upasuaji.
Aidha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Alhamisi, ya Agosti 21, 2014, ameweka
historia nyingine katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro wakati aliposafiri kwa
treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ikiwa ni mara yake ya
kwanza kutumia usafiri huo katika kipindi chake cha Urais.
Rais
Kikwete, akifuatana na Mama Salma Kikwete, amesafiri kilomita 143 ndani ya
Behewa la Kirais (Presidential Coach) la T-One kwa kiasi cha saa tatu na dakika
25 akitokea stesheni ya Ifakara katika Wilaya ya Kilombero kwenda Stesheni ya
Kisaki, Wilaya ya Morogoro vijijini.
Baada
ya hapo Rais kikwete anatarajiwa kuwasili wilayani kilosa august 24 mwaka huu
siku ya ijumapili na atazindua miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa umeme katika
kata ya kisanga na kuzindua barabara ya lami kutoka Dumila wilayani kilosa hadi
Rudewa wilayani kilosa na kufuatiwa na kuongea na wananchi wa wilayani kilosa.
No comments:
Post a Comment