Wakulima wa wilayani kilosa mkoani
morogoro wailalamikia serikali kwa kutowajali kutokana na mifugo kuingia
kiholela wilayani humo na kuharibu mazao yao mashambani mwao.
wananchi wakiwa kwenye majadiliano kwenye mkutano juu ya usuluhishi wa kuvamiwa na mifugo kijijini hapo
Wakizungumza katika mkutano wa
kijiji august 19 mwaka huu baadhi ya wakulima wa kijiji cha ulaya mbuyuni
Timotheo Mahembula,Saidi Hamisi na Zena kondo Wamesema kuwa wanapata manyanyaso
kutoka kwa wafugaji hao kutokana na kulishiwa mazao yao mashambani na viongozi
kutotoa msaada wowote kwao,na wameongeza kwa kusema kuwa tarehe 12 august ya
mwaka huu walikaa kikao na kuahidiwa na Afisa Tarafa Raphael Mvurungu kuwa
baada ya siku saba [7] watapatiwa majibu sahihi juu ya mgogoro uliopo kati ya
wakulima na wafugaji katika kijiji hicho lakini haikuwa hivyo kutokana na siku
hiyo ya saba viongozi hao kutoonekana katika mkutano huo wa wakulima.
Mifugo ikiwa shambani ikishambulia mazao aina ya mbaazi
Wameongeza kwa kusema kuwa kwa
sasa hawana Imani na viongozi wa kijiji chao kutokana na viongozi hao kushindwa
kuwaondoa wafugaji katika kijiji chao na kutowasikiliza wakulima kuhusu kilio
chao cha mifugo kuingia mashambani na kula mazao yao.
Aidha kwa upande wake Afisa
tarafa wa Tarafa ya Ulaya Raphael Mvulungu amesema kuwa yeye hakufika katika
kikao hicho kutokana na tatizo hilo kuendelea kulitafutia ufumbuzi Zaidi na
uliosahihi na ameongeza kuwa wananchi waondoe hofu kwani mgogoro huo utakwisha
na wakulima wataendelea na shughuli zao kama kawaida kikubwa amewataka kuwa na
mvumilivu katika kupa suluhu juuu ya tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment