Imesemekana kuwa tatizo la
wasichana kupata mimba wakiwa mashuleni linasababishwa na viongozi kutowafuatilia waliowakatisha masomo
wasichana hao wakiwa bado wapo shuleni.
Bodi ya shulewa kwanza kushoto ni mratibu elimu kata akifuatiwa na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ukwiva Liberath patrick Ngure na kufuatiwa na mwenyekiti wa bodi ya shle Mussa Hamisi na wa pili kutoka kulia na ni Afisa tarafa wa tarafa ya ulaya Raphael Mvulungu
Akizungumza katika bodi ya shule august 22
mwaka huu Mkuu wa shule ya Ukwiva Liberath Patrick Ngure amesema kuwa tatizo la wasichana
kupata mimba shuleni hapo limekuwa sugu kutokana na kila mwaka kuongezeka kwa
wasichana wanaopata mimba ambapo hadi kufikia February mwaka huu tayari
wasichana wane walionekana kuwa na ujauzito na kufikia mwezi may msichana mmoja
aligundulika kuwa ni mjamzito na kusema kuwa swala hilo kwa upande wake
amewasilisha majina kwa Afisa mtendaji kata kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi
lakini hakuna jitihada zozote zilizoonyeshwa kutoka kwa kiongozi huyo jambo
ambalo ameeleza kuwa linamkatisha tamaa.
Mwalimu mkuu wa shule ya ukwiva Liberath Patrick Ngure
Aidha ameongeza kuwa aliandika
barua yenye kumbukumbu namba USS.CS.HM.VOL11/69 iliyokuwa ikihitaji taarifa juu
ya mimba za wanafunzi wane [4]zilizoripotiwa katika ofisi ya kata na mtendaji wa kata aliahidi
kuleta namba za kesi zilizofunguliwa mahakamani jambo ambalo hajalitekeleza.
Kwa
upande wake Afisa tarafa wa tarafa ya ulaya Raphael mvulungu amesema
kuwa bodi ya shule inatakiwa kusimamia maswala ya kishule kwa makini ili
kumpa nafasi mkuu wa shule kuweza kuendesha shule kwa makini kwa kubaki
na swala la kukuza elimu shuleni hapo na si vinginevyo.
Mjumbe katika bodi ya shule Crensensia Mfanyakazi
Wakichangia mada hiyo ya
kuongezeka kwa mimba mashuleni baadhi ya wajumbe Mratibu elimu kata Robert
Mshani,Crensensia Mfanyakazi wamesema kuwa viongozi ngazi ya kata wamekuwa
wapuuziaji juu ya ufuatiliaji na utatuzi wa matatizo ya shuleni hapo jambo
ambalo linakwamisha maendeleo shuleni hapo.Mjumbe wa bodi hiyo ya shule Rubanga Mapesi
Mwisho mwenyekiti wa bodi hiyo ya
shule Mussa Hamisi kwa kushauriana na wajumbe wameamua kuunda kamati
itakayowafuata viongozi wanaoonyesha kukwamisha swala la ufuatiliaji wa
kufungua kesi mahakamani dhidi ya wale wasichana waliopata mimba.
Mwenyekiti wa bodi ya shule Mussa Hamisi
No comments:
Post a Comment