Wananchi wa kijiji cha
Ulaya mbuyuni wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wamelishukuru shirika TFLG na
Mjumita kwa kuwajengea ofisi ya kijiji kijijini hapo.
Maandalizi ya ujenzi wa ofisi ya kijiji katika kijiji cha mbuyuni wilayani kilosa mkoano morogoro
Afisa Tarafa wa Tarafa hiyo
ya Ulaya Raphael Mvulungu amesema kuwa wanalishikuru shirika hilo kwani
wamenufaika nalo kwa kiasi kikubwa kutokana na mpango ulioanzishwa kijijini
hapo wa matumizi bora ya ardhi ambapo unahusishwa na uvunaji wa hewa ukaa na
kuongeza kuwa hadi sasa kijiji kimejipatia fedha nyingi kupitia mradi huo.
Afisa tarafa wa tarafa ya ulaya Raphael Mvulungu
Naye mwenyekiti wa kijiji
hicho cha Ulaya Mbuyuni Khamisi Mjomba amesema kuwa kupitia shirika hilo kijiji
kina fedha zaidi ya shilingi milioni 41 kwenye benki ya CRDB na fedha hizo
zitatumika katika shughuli za kimaendeleo.
Mwenyekiti wa kijiji cha ulaya mbuyuni Rashid Mjomba
Na ameongeza kuwa katika
ujenzi huo wa ofisi ya kijiji gharama zote zitakuwa ni za shirika na siyo zile
fedha ambazo zimeshakusanywa.
Ujenzi wa ofisi ya kijiji ukiwa unaendelea
Naye Mwanakamati katika
ujenzi huo wa ofisi ya kijiji Comledy Robert amesema kuwa wanashukuru shirika
hilo kwani katika kijiji chao hakuna ofisi ya kijiji na ofisi inayojengwa sasa itakuwa na ukumbi wa
mikutano , mahabusu na ofisi yenyewe na amesema kuwa ujenzi huo unatarajiwa
kuanza hivi karibuni na kukamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa.
No comments:
Post a Comment