KILOMBERO PLANTATION LIMITED YATOA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI WILAYANI KILOMBERO YENYE THAMANI YA TSH M 1.75
Kituo Kidogo
cha Polisi cha Mngeta kilichopo wilayani Kilombero kimepatiwa msaada wa
pikipipiki moja aina ya bajaji Boxer yenye thamani ya shilingi 1,750,000 kutoka
kampuni ya Kilombero Plantation Limited KPL.
Meneja
Rasilimali watu wa
kampuni hiyo Bwana David Lukindo amesema kuwa msaada huo umekabidhiwa
hivi karibuni na mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Cater
Coleman.
Bwana
Lukindo amesema kuwa kampuni imetoa msaada huo baada ya kutambua kituo hicho
kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa usafiri na msaada huo na anaamini kwa
kiasi kidogo watakuwa wamesaidia katika kuimarisha ulinzi katika tarafa ya
mngeta.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa msaada wa pikipiki hiyo Mkuu wa kituo hicho Mkaguzi
msaidizi wa Polisi Joseph Elias,ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na
anawaomba wadau wengine kuiga mfano wa KPL.
Bwana Elias
amesema kuwa jeshi la polisi linakabiliwa na changamoto nyingi hususan usafiri
hali inayowafanya kushindwa kuwafikia wananchi katika maeneo mengi hivyo
kupatikana kwa usafiri huo utasaidia jeshi
hilo kupambana na wahalifu kwa kuwafikia wananchi wengi ,ili kupunguza vitendo
vya uhalifu katika tarafa ya mngeta.
No comments:
Post a Comment