WAKANDARASI WAASWA WILAYANI KILOMBERO
WAKANDARASI
wa Ujenzi Nchini wametakiwa kufanya Kazi
zao kwa kuzingatia Sheria, ubora na Kiwango cha Hali ya Juu.
Akiongea mara
baada ya kukagua maandalizi ya Awali ya Ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero
Mkoani Morogoro, Naibu Waziri wa Ujenzi Injinia
Greyson Lwenge amesema kuwa ubora wa hali ya juu unahitajika katika ujenzi
unaofanyika na makandarasi wakabidhi Daraja likiwa katika kiwango cha juu.
Amesema kuwa
jumla ya fedha Shilingi Bilioni 53 zitatumika katika kukamilisha Ujenzi wa Daraja hilo
litakalokamilika Januari 2015.
Tayari shilingi
Bilioni 8 zimekwishatolewa kwa ajili ya Mandalizi ya Awali ya Ujenzi wa Daraja
hilo linalounganisha Wilaya ya Kilombero na Ulanga.
Kivuko katika mto kilombero kikitumika kuvusha abiria,wakati wakazi wake wakisubiri kumalizika kwa daraja mwaka 2015. (picha na Henry Bernard Mwakifuna.)
Awali Injinia
Mkuu wa Kampuni ya China Railways Group wanaojenga Daraja hilo Liang Yan Ping
amesema kuwa watajenga Daraja hilo kwa Kiwango kwa kuwa wanauzoefu wa Ujenzi wa
madaraja.
Liang
amesema kuwa Muda wa Miezi 24 uliowekwa utatumika kukamilisha ujenzi huo,
ingawa wako Nyuma katika Miezi Mitatu waliopewa kwa ajili ya Maandalizi ya
Ujenzi huo.
Wakati huo
huo Naibu Waziri wa Ujenzi Injinia Greyson Lwenge amesema kuwa Barabara ya
Mikumi, Ifakara, Lupiro hadi Lumecha Mkoani Ruvuma ipo kwenye mchakato wa
kupata Wakandarasi watakaoiwekea Lami.
Amesema kuwa
Barabara hiyo yenye Urefu wa Kilomita 512 ni muhimu kwa Mkoa wa Morogoro na
Taifa kwa Ujumla inataraji kuwa katika Kiwango kizuri ifikapo Mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment