Mazishi ya Mkazi Mmoja wa Kibena Mjini Njombe bwana Mexon Nyekelela Chota
Yamefanyika Katika Makaburi ya Kibena,Ikiwa ni Baada ya Kupatikana
Kwa Mwili wa Marehemu Uliokuwa Amezama Kwa Siku ya Tano Katika Mabwawa
ya Kampuni ya TANWAT Mjini Njombe.
Akizungumza Mara Baada
ya Kupatikana Kwa Mwili Huo Afisa Tarafa ya Njombe Mjini Bi Lilian
Nyemele Ameishukuru Kampuni ya TANWAT Kwa Namna Ilivyoshiriki Katika
Kusaidia Zoezi Hilo Pamoja na Wananchi Wote Walioshiriki.
Mwili wa Marehemu Ulipatikana
Leo Majira ya Saa Nane Mchana Ikiwa ni Baada ya Jitihada za Muda Mrefu
za Wananchi na Viongozi Kuweza Kuutafuta Mwili Huo Bila Mafanikio
Kutokana na Ukosefu wa Vifaa Vya Uokozi.
Akizungumza
Mara Baada ya Kuwasili Mkoani Njombe Mtaalam wa Uzamiaji Kutoka Jijini
Dar Joseph Mapunda Anasema Kuna Haja Kwa Serikali ya Mkoa wa
Njombe Kuanza Kutoa Mafunzo Kwa Wananchi na Wataalam Mbalimbali Ili
Kuweza Kupata Wataalam wa Uzamiaji.
Marehemu Mexon Nyekelela
Chota Alizama Kwenye Mabwawa Hayo Mnamo March Mosi Mwaka Huu Majira ya
Saa Kumi na Moja Jioni Wakati Akiwa na Wenzake Mara Baada ya Kumaliza
Shughuli Zao za Sanaa.
No comments:
Post a Comment