WANANCHI WA KIJIJI CHA MCHOMBE WAWAONDOA VIONGOZI WAO WA SERIKALI MADARAKANI.
Wananchi wa
Kijiji cha Mchombe wamewaondoa madarakani viongozi wa serikali ya kijiji
hicho katika mkutano wa kijiji kutokana
na kuhusika na upotevu wa fedha jumla ya shilingi 2,190,000.
Kaimu Afisa
Tarafa wa Tarafa ya Mngeta Bwana Shabani Mgaya amesema kuwa Kuondolewa
madarakani kwa serikali hiyo kumetokana na taarifa ya mkaguzi wa ndani wa
hesabu za serikali kubaini makosa
mbalimbali yaliyofanywa na serikali hiyo.
Amesema
serikali hiyo imefanya upotevu wa shilingi 2,190,000 ambazo zimepotea kwa
uzembe wa viongozi hao ambapo shilingi 1,780,000 ilitolewa benki na ilitumika
bila ya idhini ya serikali.
Aidha Bwana
Mgaya amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi imeeleza kuwa kati ya fedha
hizo shilingi
300,000 zilitokana na uuzwaji wa ardhi
ya kijiji ambapo ni kinyume na sheria kwani ardhi hiyo iliuzwa bila ya kufuata
taratibu na pesa hiyo haikuonekana.
Taarifa hiyo ya mkaguzi ambayo imewafanya
wananchi kuuondoa uongozi madarakani imeeleza kuwa shilingi 1,100,000 fedha
kutoka mfuko wa jimbo ambayo ilikuwa kwa ajili ya uchimbaji wa visima imetumika
kwa matumizi mengine tofauti na yaliyokusudiwa.
Aidha miongoni mwa mambo yaliyobainika katika
taarifa ya mkaguzi wa ndani kwa viongozi
wa serikali hiyo ni udhaifu wa serikali katika kukusanya mapato,udhaifu wa
kutosimamia shughuli za maendeleo na kutosoma taarifa za mapato na matumizi kwa
vipindi vitatu mfululizo.
No comments:
Post a Comment