WAANGOLA KUCHEZESHA MECHI YA STARS
Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Angola
kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Morocco (Lions of the Atlas).
Mechi hiyo ya
kundi C itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Ivory Coast ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne na
kufuatiwa na Taifa Stars yenye pointi tatu.
Mwamuzi wa
mechi hiyo ni Helder Martins de Carvalho wakati mwamuzi msaidizi namba
moja ni Inacio Manuel Candido huku Ricardo Daniel Cachicumi akiwa
mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni
Antonio Muachihuissa Caxala.
Waamuzi hao
watawasili nchini saa 1.20 usiku Machi 22 mwaka huu kwa ndege ya Kenya
Airways wakitokea Luanda, Angola kupitia Nairobi, Kenya.
Kamishna wa
mechi hiyo atakuwa David Fani kutoka Botswana anatarajiwa kuwasili Machi
22 mwaka huu saa 1.45 usiku kwa ndege ya South African Airways.
Naye
mtathmini wa waamuzi (referee assessor) Neermal Boodhoo kutoka Afrika
Kusini atawasili nchini Machi 22 mwaka huu 1.45 usiku kwa ndege ya South
African Airways.
No comments:
Post a Comment