MECHI YA RUVU SHOOTING, YANGA YAINGIZA MIL 62/-
Mechi ya Ligi
Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Yanga iliyochezwa jana Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 62,228,000 kutokana na watazamaji
10,929.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 146 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi
wa bao 1-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku
kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,336,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,492,406.78.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,289,880.48,
tiketi sh. 4,136,390, gharama za mechi sh. 4,373,928.29, Kamati ya Ligi
sh. 4,373,928.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,186,964.14, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
850,486.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
850,486.06.
No comments:
Post a Comment