MBUNGE WA JIMBO LA KILOMBERO MH.ABDUL MTEKETA ATOA VITABU 200 VYA MASOMO MBALIMBALI KATIKA SHULE YA SEKONDARI KIYONGWILE
MBUNGE wa Jimbo la Kilombero
Mheshimikwa Abdul Mteketa ametoa msaada wa Vitabu 200 vya Masomo mbalimbali kwa
Shule ya Sekondari ya Kiyongwile iliyopo Kata ya Ifakara.
Akizungumza na Wanafunzi na Walimu
wa Shule hiyo Wakati akikabidhi msaada
huo Mheshimiwa Mteketa amewaeleza kuwa
Lengo la msaada huo ni kuinua
Taaluma na kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi
wa shule hiyo na pia ni moja ya kutekeleza ahadi ya kuboresha Elimu kwa
shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Kilombero.
Amewataka Wanafunzi na Walimu kuvitunza
Vitabu hivyo ili Viwasaidie wanafunzi waliopo kwa sasa na watakaokuja baadaye.
Msaada uliotolewa ni Vitabu vya
Masomo ya Fizikia, Kemia, Jiografia, Baiolojia na Hisabati.
Mbali na Msaada huo Mbunge huyo
ametoa Msaada wa Kalamu za Wino na Mkaa zenye Thamani ya Shilingi Laki Moja na
Elfu Hamsini (150,000/=)kwa shule ya Msingi ya Lipangalala huku akiwaahidi
kujenga Vyoo na kuweka Maji katika Shule hiyo.
Mheshimiwa Mteketa ametoa ahadi hiyo
baada ya uongozi wa shule hiyo kumweleza matatizo hayo likiwemo na tatizo la Ukosefu wa Umeme shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment