WATOTO WA KITUO CHA BETHELEHEMU KILOMBERO WAPATIWA ZAWADI YA SIKUKU YA PASAKA.
Wanawake wa
kata ya Kibaoni Wilayani Kilombero wametoa msaada wa mbuzi wawili kwa ajili ya
sikukuu ya pasaka kwa watoto walemavu wa akili wa kituo cha bethelehemu unaogharimu
jumla ya shilingi 180,000.
Akizungumza
wakati akikabidhi msaada huo Mratibu wa kamati ya sherehe ya siku ya mwanamke
duniani Bi Sophia Msiku amesema kuwa msaaada huo umepatikana baada ya wanawake
hao kufanya harambee katika sherehe ya siku ya wanawake duniani.
Bi Msiku
amesema kuwa katika kusherekea siku ya mwanamke duniani walipanga kushiriki na
watoto hao lakini kutokana na mambo kuingiliana walishindwa kufanya hivyo na
badala yake walipanga siku ya kupeleka msaada huo.
Akizungumza
wakati akipokea msaada huo mlezi mkuu wa kituo hicho Sister Maria Dorothea
Lyimo amewashukuru akina mama hao na amewataka watu wengine kuiga mfano huo kwa
kutoa msaada huo kwa watoto hao .
No comments:
Post a Comment