SIKU YA MWANAMKE
DUNIANI
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Bi Azimina Mbilinyi anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambayo
yataadhimishwa na wanawake wa kata ya
Kibaoni katika viwanja vya soko la Kibaoni.
Mratibu wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo Bi Sophia
Msiku ambae ni Afisa Mtendaji wa kata hiyo amesema kuwa kata ya kibaoni
imejipanga vizuri katika maadhimisho hayo .
Bi
Msiku amesema kuwa maadhimisho hayo
yataanza kwa maandamano kuanzia maendeeleo na maandamano hayo yatapokelewa na
Mgeni rasmi katika viwanja hivyo.
Amesema
katika maadhimisho hayo kutakuwa na maonyesho ya sanaa,michezo mbalimbali,na
pia wanawake watatoa ushuhuda mbalimbali.
Ameongeza
kuwa Mbali na kutoa ushuhuda mbalimbali pia
elimu ya watu kujua haki zao katika kupambana na rushwa itatolewa
Kauli mbiu
ya maadhimisho hayo inasema kuwa uelewa wa masuala ya jinsia katika
jamii,ongeza kasi.
No comments:
Post a Comment