WANAFUNZI WILAYANI KILOMBERO WAHIMIZWA KUONGEZA BIDII KATIKA MASOMO YAO
Wanafunzi
wilayani Kilombero wamehimizwa kuongeza bidii katika masomo ili wafanye vizuri katika mitihani yao ya kumaliza kidato
cha nne na kuondokana na aibu ambayo taifa imepata kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kwa mwaka 2012 kufeli.
Hayo
yameelezwa leo na mbunge wa jimbo la Kilombero Mheshimiwa Abdul Mteketa wakati
akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Kibaoni alipokuwa
akitoa msaada wa vitabu 100 vya masomo ya hesabu,jiografia,kemia,fizikia na
bailojia katika shule hiyo.
Mh,Mteketa
amesema kuwa kufeli kwa wanafunzi wengi inatokana na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya upungufu wa vitabu ,walimu na baadhi ya wanafunzi kutokuwa na
nidhamu hivyo amewataka wazazi ,walezi
na walimu kushirikiana kikamilifu ili
kuinua kiwango cha taaluma shuleni hapo .
Kuhusu
baadhi ya wanafunzi kutokuwa na nidhamu kwa walimu na utoro,amesema suala la
nidhamu kwa mwanafunzi ni ushirikiano kati ya wazazi na walimu na hivyo
amewataka wazazi kuwa wakali kwa watoto wao pindi wanapokosea badala ya kuwatetea , hali hiyo inasababisha
wanafunzi wengi kutokuwa na nidhamu pindi wanapoona wanatetewa na wazazi wao.
Awali
akizungumza wakati akipokea msaada huo kwa niaba ya shule mkuu wa shule
hiyo Bwana Zakaria Kalinga amemshukuru
Mh Mteketa kwa msaada wa vitabu 100 na
amemuomba asichoke kuitembelea shule hiyo na kutatua changamoto zinazowakabili
ili kuinua kiwango cha taaluma shuleni hapo.
Bwana
Kalinga amesema shle hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa
vitabu,uchache wa samani za ofisi,uhaba wa walimu hasa wa masomo ya
sayansi,ukosefu wa nyumba za walimu,ukosefu wa hostel na ukosefu wa vifaa vya
michezo na fedha kwa ajili ya matengenezo ya uwanja .
Kuhusu vifaa
vya michezo na matengenezo ya uwanja mbunge huyo amewaahidi atahakikisha anatekeleza ahadi
hiyo.
No comments:
Post a Comment