WAKULIMA WILAYANI KILOMBERO WALALAMIKIA UCHELEWESHWAJI WA MBOLEA ZA RUZUKU .
Wakulima wa
vitongoji vya lipangalala,lihami,kwa mkuya na kiyongwile kata ya Ifakara
Wilayani Kilombero wamelalamikia kucheleweshwa mbolea ya ruzuku ambayo ilitakiwa kufika tangu mwezi wa kumi na
mbili mwaka jana.
Wakizungumza
na Mtandao huu wa habarikwanza Baadhi ya wakulima wamesema kuwa pembejeo katika maeneo hayo
zimechelewa kufika hali ambayo imewafanya wakulima hao kushindwa kuzitumia hasa
zile za kupandia kutokana na muda kupita.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kamati ya kugawa vocha za pembejeo katika maeneo hayo Bwana
Paulo Magehema amekiri malalamiko ya wakulima hao ambapo amesema kuwa mbolea
hiyo ilitakiwa ifike mwaka jana lakini imefika mwezi machi mwaka huu huku
mimea ikiwa imeshaota na kukua hivyo kwa upande wa mbolea ya kupandia
haitafanya kazi yoyote.
No comments:
Post a Comment