MBUNGE WA MULEBA KASKAZINI MHESHIMIWA MWIJAGE KUWASAIDIA WAPIGA KURA WAKE
Serikali imetoa jumla ya tani 160 za
chakula na fedha taslimu shilingi milioni sitini zimetolewa na Waziri mkuu
Mizengo Peter Pinda kwa waathirika wa mafuriko
yaliyotokea march 28 katika vijiji vya kata ya Ibuga Wilaya ya
Muleba Mkoani Bukoba.
Vijiji vilivyoathiriwa na maafa
hayo makubwa ambayo yamesababisha nyumba takribani 150 kuezuliwa na
upepo na watu kukosa makazi na mazao kuharibika ingawa hakuna aliyekufa
na kujeruhiwa katika tukio hilo
Akizungumza na wananchi wa kijiji
hicho katika ziara yake Mbunge wa Jimbo la Muleba kaskazini mheshimiwa Mwijage
amesema amesikitishwa sana baada ya kupata habari hizo kwani ni mara ya pili
kutokea kwa maafa hayo, kwa kuwa maafa kama
hayo yalishawahi kutokea mwaka 2012 hivyo amewapa pole wanakijiji hao na
kuwataka kutokata tama kwa hali hiyo.
Mheshimiwa Mwijage amesema baada ya
kutembelea vijiji hivyo amebaini karibu nyumba 150 zimeezuliwa na upepo
na baadhi familia kukosa makazi pamoja na mazao kuharibiwa vibaya
hivyo ametoa bahasha kwa kila muathirika akidai kuwa ina misumari ndani yake na
kuwakilisha msaada uliotolewa na serikali ikiwa ni tani 160 za chakula na
msaada kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na milioni 60 alizotoa kwa ajili ya
kununua maharage kwa wanakijiji hao.
Mwijage pia amewaahidi wanakijiji
hao kuwa wataletewa mahindi ambayo watauziwa kwa bei ya shilingi hamsini
kwa kilo lakini pia ametoa misaada ya papo hapo kama fedha tasilimu kwa ajili
ya malipo ya ada kwa wanafunzi walioshindwa kwenda shule kutokana na hali
hiyo.Baadhi ya misaada mingine ni sare za shule,mabati kwa bahadhi ya
wanakijiji ,na kutoa tamko kwa wakuu wote wa shule kutokudai ada kwa
wanavijiji hivyo mpaka itakapofika mwezi November mwaka huu na
amechukua jukumu la kuwasomesha watoto wote waliofanya vizuri katika masomo yao
ya kidato cha nne mwaka huu .
Akitoa angalizo kwa wale ambao
wamekuwa wakitumia maafa hayo kwa manufaa yao binafsi kwa kuomba misaada toka
sehemu mbalimbali kwa kutumia jina la kijiji cha Buhembo bila kupata kibali
maalumu kutoka katika uongozi maalumu na kusema kuwa huo ni wizi na wenye
tabia hiyo waache na kufuata utaratibu unaohusika
Wakipokea misaada hiyo nao
wanakijiji wa vijiji vya kata ya Ibuga wamesema wanaishukuru serikali kwa
kuwapa misaada hiyo kwani wamekuwa katika hali ngumu sana na kumshukuru mbunge
wa jimbo hilo kwa kuchukua jukumu la kuwasomesha watoto wao