Zoezi la kumtafuta mwanafunzi wa shule ya sekondari
Kilosa alietumbukia kwenye maji na
kupotea katika mto wami bado linaendelea katika kijiji cha Ludewa gongoni Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
Akizungumza na HABARIKWANZA mwalimu Mkuu wa shule hiyo Erasto Lulandala
amesema kuwa mwanafunzi aliyetambulika kwa
jina la Protasi Masinde Stansilaus mwenye umri wa miaka 14 alitumbukia
mtoni sehemu yenye kina kirefu mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumzia tukio
hilo mwalimu huyo aliongozana na wanafunzi wenzake wawili waliojulikana kwa
majina Julias Mathias na Kapungu Kiwangu wanaokadiliwa kuwa na umri wa miaka 14
ambapo walienda mtoni kuchota maji ya
kuoga na ndipo mtoto huyo alipotumbukia kwenye maji na kupotea.
Kwa upande wake Baba Mkubwa wa mwanafunzi huyo
Raimond Tungaraza amesema kuwa matumaini
ya kumpata mtoto ni mdogo kwani tangu apotee ni
siku ya tano na hali ya hewa inazidi kuwa mbaya kwani mvua zinanyesha na
maji yanaongezeka kila siku. Tungaraza amesema kwa sasa wanaendelea
kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Rudewa gongoni kikosi cha uokoaji pamoja
na askali polisi kumtafuta mwanafunzi huyo.
Naye kamanda wa polisi mkoani Morogoro Faustine
Shilogile amesema kuwa tukio hilo la mtoto kupotea kwenye maji kuwa hawezi
kutoa majibu kama amefariki au laa na majibu zaidi yatapatikana hadi pale
atakapopatikana.
No comments:
Post a Comment