Mabaki ya mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza
katika shule ya sekondari kilosa aliyefahamika kwa jina la Protas masinde
yameonekana April 26 katika mto wami rudewa
.
Akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya kilosa Elias
Tarimo amesema kuwa mtoto huyo amepotea tangu April10 ya mwaka 2014 na juhudi
za kumtafuta hazikuzaa matunda.
Aidha Tarimo ametoa wito kwa wanafunzi kufuata maelekezo pindi
wawapo shuleni kwa kueleza kuwa marehemu na weenzake wawili walitumwa kuchota
maji iliyo salama lakini wao walienda sehemu nyingine na kusababisha madhara
hayo.Pia ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na miundombinu ya maji kuharibiwa
na mto shuleni hapo na kuwalazimu wanafunzi kwenda kuchota maji mtoni kwa ajili
ya shughuli mbalimbali pia Halmashauri ya wilaya ya kilosa imejipanga
kukarabati miundombinu hiyo ili kuepusha usumbufu na upatikanaji wa maji
shuleni hapo.
Pia Baba mkubwa wa mototo Raimond Tangaraza amesema
wamesikitishwa sana na taarifa hiyo lakini amesema kuwa kazi ya mungu haina
makosa na licha majonzi hayo anawashukuru viongozi,wananchi na
majirani kwa msaada wao waliouonyesha katika utafutaji wa mwili huo wa mototo
wao.
Aidha mwalimu mkuu wa shule hiyo Erasto Lulandara amesema
kuwa mwanafunzi huyo amepatwa na umauti huo alipoenda kuchota maji akiwa na
wenzake sehemu ambayo maji yanachemka na amesema kuwa ni sehemu yenye kina
kirefu ndipo Protas alipotumbukiza ndooyake kwa ajili ya kuchota maji ndipo
ndoo ikamtereza na na alipojaribu kuidaka ndipo alopotereza na kuzama majini.
Kwa upande wake shuhuda wa tukio hilo Saidi Ally amesema
kuwa wamekuta mwili wa marehemu ukiwa ni vipandevipande abavyo ni fuvu la
kichwa,mikono na sehemu ya mwili na kusema kuwa chanzo cha kugunduliwa kwa
mwili huo watoto waliokuwa wanavua samaki katika mto huo ndipo walipounasa
mkono wa marehemu na kuongeza kuwa wameukuta mwili huo ukiwa katika hali mbaya.
Naye mganga mkuu wa hospitari ya wilaya ya kilosa John
Nkinda amethibitisha kuwa ameupokea mwili huo ukiwa katika hali ya
vipandevipande majira ya saa 8 mchana ya April 26 na kueleza kuwa wameuhifadhi
chumba cha kuifadhia maiti na wanawasubiri
ndugu wa motto huyo kuja kuchukua mabaki ya mwiliwa marehemukwa ajili ya
shughuli za mazishi.
Aidha kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Paulo Leornad
amesema kuwa amepokea taarifa hizo april 27 na kuahidi kutolea maelezo April 28
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment