Tuesday, April 1, 2014

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 13 AFA MAJI WILAYANI KILOSA



Mtoto mwenye umri wa miaka 13 Juma Nurdin mwanafunzi wa darasa tatu shule ya msingi kichangani wilayani kilosa amekufa maji march 31 wakati alipokuwa akioga na wenzake katika madimbwi.

Akielezea tukio hilo Bibi wa motto huyo Rhoda John amesema kuwa mtoto huyo aliondoka na wenzake kwenda kuoga pasipo yeye kujua na ndipo alipoletewa taarifa na wenzake kuwa motto huyo amefariki.
 
Aidha kaka wa marehemu naweka juma amesema kuwa alimkataza mdogo wake kwenda kuoga katika madimbwi hayo kutokana na marehemu kuwa na matatizo ya ugonjwa wa kuanguka[kifafa]lakini marehemu alipoona wenzake wanaoga naye aliamua kuoga na kukutwa na umauti huo.

Kwa upande wa mashuhuda wa tukio hilo Rajabu Shomvi amesema kuwa tukio hilo ni la tatu kutokea katika kitongoji hicho na yote yakiwa ni kutokana na maradhi ya ugonjwa huo wa kuanguka na kuwataka wananchi wenzake kuwa makini na watoto.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa kitongoji cha manzese B Kata ya mkwatani wilayani kilosa mkoani morogoro Hamisi Mwasambila amesema kuwa tukio hilo ni la pili kutokea tangu yeye aingie madarakani mwaka 2009 na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wadogo na wale wenye matatizo yaugojwa wa kuanguka na wenye matatizo ya akili na kuwataka wananchi kuacha kufyatua matofali karibu na makazi ya watu.

No comments:

Post a Comment