Mkazi wa
kijiji cha manembo kitongoji cha Mng’ongo wilaya mvomero mkoani Morogoro
Theresia Herry mwenye umri wa miaka 80 amefariki baada ya kusombwa na maji
katika mto mseleleko mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumzia mazingira ya kifo hicho mtoto wa marehemu
Martin Cosmas amesema kuwa mama yake alienda shamba siku ya ijumaa akiwa
ameongozana na Dada yake Serapia Cosmas na baadaye walipokuwa wanarudi
walipofika mtoni Bi, Theresia alipokuwa anajaribu kuvuka alisombwa na maji hayo na mwanaye aliyekuwa
naye alipojaribu kumuokoa alishindwa kutokana na maji hayo kuwa na nguvu na
ndipo marehemu alipokutwa na umauti huo.
Aidha mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Charles Golaga amesema
kuwa wameshtushwa na kusikitishwa sana
na msiba huo kwa kusema kuwa marehemu alikuwa hajaumwa na alikuwa anatoka
shamba ndipo akakutwa na umauti huo.
Naye
mwenyekiti wa kijiji cha mng’ongo amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mto huu ni mara ya kwanza
kusababisha tukio hilo na kuongeza kwa
kusema kuwa anawataka wananchi
kuwa makini na maji yanayotiririka mtoni
na kuacha tabia kujaribu kuvuka maji yenye kina kirefu na yenye kasi.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani Morogoro
Faustine Shilogile amesema kuwa tukio hilo bado halijawafikia na kuahidi
kulifuatilia.
No comments:
Post a Comment