Imeelezwa kwa zaidi ya kaya 208 za kitongoji cha
Rozi kata ya magomeni wilyani kilosa hawana mahali pa kuishi kutokana na mafuriko yaliyotokea yametokana na mvua zinazoendelea kunyesha
wilyani humo.
Hayo yameelezwa april 9 mwaka 2014 na
mwenyekiti wa kitongoji cha Rozi Bw
Abdul Bona wakati akiongea na HABARI KWANZA
ofisini kwake na kusema kuwa anaiomba serikali kuwatengea eneo maalum
wahanga hao wa mafuriko. Bw Bona amesema kuwa
wahanga hao kwa sasa wanishi kwa zao na wengine wanaishi katika nyumba ambazo
zimebomolewa hivyo wanahitaji msaada.
Pia ameomba watendaji wa ngazi za juu kushirikiana
na serikali za vijiji hasa katika majanga kama haya ameongeza kuwa katika
mafuriko ya mwaka 2009/2010 serikali iliwaombia wahanga watawapatia sehemu ya
kuishi jambo ambalo halijatekelezwa mpaka sasa.
Amesema anaomba serikali kuwaangalia wahanga hao kwa
jicho la tatu kwani mvua bado zinaendelea hivyo hawajui siku za usoni hali
itakuwaje.
Barabara zikiwa zimejaa maji
No comments:
Post a Comment