MASHINDANO YA
MAIMOSI MKOANI MOROGORO
KITAIFA:
Na
Jonathan Tossi - Jeshi La
Polisi.
Katibu mkuu wa
wizara ya mambo
ya ndani nchini
Mohamed Abdulluwakily amewapongeza
wanamichezo wa wizara hiyo
na kuwaaasa kuwa michezo nisehemu ya
kazi hivyo waendelea
kushiriki michezo hiyo
kwa hali na mali. Pia
amesema kinachoitajika sasa ni
kuunda timu moja kutoka idara za
wizara ya mambo
ya ndani ya
nchi na kuwa na
timu moja ya
wizara.
Aidha kwa mara
nyingine tena Wizara ya mambao
ya ndani ya nchi
imeendelea kufanya vema katika
mbio ndefu za
umbali wa kilomita
kumi zilizo fanyika
nje kidogo ya
mkoa wa morogoro katika Barabara
ya Dar es
salaam na Zambia
majira asubuhi ya
leo toka kijiji
cha Mindu mpaka
Kijiji cha Rombo
umbali wa kilomita kumi
washiliki katika mashindano hayo
ni wizara mambo
ya ndani, wizara ya
uchukuzi Idara ya
Polisi ,Uhamiaji na
Kampuni ya TTPL ya
Mkoani morogoro
Washindi katika
mbio hizo ni
wizara ya mambo
ya ndani ambayo imewakilishwa na
wakimbiaji wakimataifa Fabian
Frank na Mariam
Abubakali huku Fabiani
akiibuka mshindi wa kwanza
na Mariam kuwa
mshindi wa kwanza
kwa wanawak.
Aidha katika
michezo mingine ya
bao karata na
drafti wizara ya
mambo ya ndani
inaendelea kufanya vema
katika michezo hiyo
huku mchezo wa drafti
ukiendelea muda huu katika
viwanja vya jamhuri
hapa morogoro
Pia
katika michezo ya
netball yaani mpila wa pete
timu ya mambo ya ndani
inashuka ndimbani hapo kesho
majira ya saa tisa
za mchana kwa mchezo wa
huo.
No comments:
Post a Comment