Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kilosa Masalu Mayaya amewataka madereva wanaoendesha vyombo vya moto kufuata
kanuni na taratibu ya barabara.
Ameyasema haya wakati akizungumza na HABARIKWANZA kuhusu
ujenzi wa uzio wa Shule ya
Msingi Mazinyungu ambao
unagharimu kiasi cha shilingi milioni miamoja arobaini na saba miambili
themanini na tano na mia nane thelathini elfu na kusema kuwa ujenzi huo kwa sasa upo kwenye utaratibu
na kusema kuwa bado hakuna fungu la fedha kwa ajili ya ujenzi huo kwa sasa na kuwaomba
wadau kujitokeza kwa ajili ya kuweza kufanikisha shughuli za ujenzi huo.
Pia Mayaya amesema kuwa kutafanyika utaratibu kwa
ajili ya kuweka matuta katika eneo hilo la shule ya msingi mazinyungu ili
kuzuia kutokea kwa ajali eneo hilo, pia ameongeza kwa kusema kuwa madereva
waendelee kupewa elimu kuhusu matumizi ya barabara.
Naye Mkuu wa Shule hiyo ya Msingi Mazinyungu Lameck Mkude amesema
kuwa shule hiyo inakitengo maalumu cha watoto walemavu wapatao 74 wavulana 44 ,
wasichana 30 amesema kuwa wanahitaji uzio kwa ajili ya usalama wa watoto hao na
mali zao. Pia Mkude amesema kuwa pindi ujenzi wa uzio huo utakapokamilika
utafanya mali za shule na watoto hao kuwa salama kutokana na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na watoto hao.
Na kuongeza kuwa kitengo hicho cha watoto walemavu kuna watoto wenye ulemavu wa
ngozi (albino) ambapo kuna baadhi ya watu
kuwa na imani potofu.
No comments:
Post a Comment