Wakazi wa wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wanakabiliwa na
uhaba wa mafuta ya taa takribani wiki tatu kutokana na upatikanaji wa mafuta
hayo kuwa mgumu.
Akiongea na Clouds fm mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo
Kilosa Ally Malingo amesema kuwa amethibitisha kwa kusema kuwa upatikanaji wa
mafuta ya taa umekuwa mgumu na kuongeza kwa kusema kuwa ameongea na mmiliki wa
sheli ya ya mafuta Hemedi Bakhamisi na
kusema kuwa mafuta hayo ya taa yatapatikana wiki hii.
Naye mmiliki wa sheli hiyo ya mafuta ya taa bakhamisi amesema
kuwa upatikanaji wa mafuta umekuwa mgumu kutokana na baadhi ya makampuni
yanayoagiza mafuta nje ya nchi kuacha
kuagiza mafuta hayo na kuongeza kuwa mafuta yatapatikana mapema wiki hii na
kusema kuwa wanahofia kuchelewa endapo daraja la Ruvu (Kibaha) halitakuwa tayali
.
Aidha mfanyabiashara wa mafuta hayo aliyejitambulisha kwa jina moja la Alex
amesema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wamepandisha bei ya mafuta kwa
kuuza shilingi mia tatu kwa koroboi moja badala ya shilingi mia na hamsini na
kuongeza kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na upatikanaji wa mafuta hayo
kuwa mgumu.
Pia Bi Mwanaisha Mundo ambaye ni mkazi wa Kilosa amesema
kuwa upatikanaji wa mafuta kuwa mgumu umewafanya wao kulala giza , pia
ameongeza kwa kusema kuwa mafuta yanayopatikana madukani yanapatikana kwa
gharama kubwa na kusema kuwa licha ya gharama kuwa kubwa lakini upatikanaji wa
mafuta hayo bado ni mgumu
No comments:
Post a Comment