Afisa Misitu wa Wilaya ya Kilosa Othman Haule ameitaka
Serikali kuwekeza katika sekta ya mali
asili na misitu kwani ni sekta nyeti nchini.
Ameyesema hayo ofisini kwake wakati akizungumzia jinsi
misitu inavyoathiliwa na wananchi kwa matumizi ya Kila siku na kusema kuwa
chanzo cha misitu hiyo kuharibika ni kutokana na serikali kutoipa kipaumbele
sekta hiyo ya maliasili na kusema kuwa changamoto inayowakabili ni baadhi ya wananchi kutokujua
umuhimu wa misitu na kuitumia vibaya kwa uchomaji mkaa hovyo kilimo ndani ya
misitu , pamoja na ufugaji horela na kutolea mfano
msitu wa mamiwa kisara North ulivyohalibiwa kwa shughuli za Kilimo
pamoja na misitu ya Gairo ilivyoharibiwa kwa Ufugaji horela wa mifugo na
uchomaji wa mkaa na kusababisha eneo hilo kuwa jangwa.
Pia amewaasa wananchi wanaokaa pembezoni mwa misitu kuacha kufanya shughuli za uhalibifu wa msitu ikiwemo uchomaji moto kwa ajili ya uwindaji shughuli za kilimo pamoja na uchomaji wa mkaa. Na kuongeza kwa kusema kuwa anawataka wananchi kuitunza vizuri misitu ili kuweza kuendelea kupata mvua kwa wingi na kuondokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo kwa sasa.
Tanki la maji likiwa likiwalimekauka kutokana na ukame uliopo sehgemu hiyo uliotokana na ufugaji horela na uchomaji wa mkaa.
Mashamba yakiwa katikati mwa msitu wa mamiwa kisara North kata ya lumbiji wilayani kilosa.
Aidha amesema kuwa kila mwananchi anajukumu la kutunza
misitu kwa kusema kuwa mwananchi anapoona magunia ya mkaa barabarani akae
akitambua kuwa kuna misitu imeteketea na kusisitiza kuwa kila mwananchi
anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake.
biashara ya mkaa maguha yazidi kuteketeza misitu wilayani gairo
No comments:
Post a Comment