Wakazi wa kata ya mbumi A wilaya ya Kilosa mkoani
morogoro wameilalamikia serikali kwa kutowafanyia marekebisho mifereji ya
kupitishia maji na makaravati kwa kutokuwa na ubora.
Hayo yameelezwa April 10 mwaka huu wanakijiji wa
Mbumi “A” kata ya Mbumi wilayani Kilosa , waliovamiwa na maji yaliyopasua
kutoka mifereji na kusababisha madhara katika makazi yao.
Aidha baadhi ya wanakijiji hao waliothilika na maji
hayo Ally Nassoro Mkelewe na Magreth Msonge wamesema kuwa wametoa malalamiko
yao kwa muda mrefu lakini serikali bado haijawatekelezea mahitaji yao kwa kusema kuwa makaravati yaliyopo yapo
chini ya kiwango kwani yaliyopo ni makaravati yenye urefu wa CM 60 na machache ni ya cm 90 . Na kuongeza kuwa
makaravati yanayohitajika ni yale yenye urefu mzuri wa kupitisha maji kiurahisi.
Aidha mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi “A” Ally .S.
Ngata amesema kuwa wakazi wake wameathiliwa na maji hayo na kueleza kuwa
zinahitajika jitihada za karaka kuweza kuokoa mali za watu pamoja na
miundombinu na kuongeza kuwa anawaomba waandisi kutembelea eneo la kwa Ngola
kuona jinsi maji yanavyopita kwa urahisi kutokana na mfereji kuwa mrefu na
karavati zenye ubora zenye uwezo wa kupitisha maji mengi kwa haraka.
Naye mwenyekiti wa mji mdogo Kilosa Ally .S. Malingo
amesema kuwa maji yanayowasumbua wakazi wa mbumi “A” ni yale yale yanayotoka manzese ambapo
kulikuwa na miti mingi na ilikuwa inapunguza maparomoko ya maji ambapo kwa sasa
kuna makazi ya watu na kusababisha maji kuporomoka kwa kasi na karavati
zilizopo kushindwa kuhimili maji . Aidha Malingo amesema kuwa ifikapo june
mwaka huu serikali itaanza ukarabati wa maeneo yaliyoharibika na kuwataka wanakijiji
kuwa na uvumilivu kwa kipindi hiki.
No comments:
Post a Comment