Imeelezwa kuwa wakazi wa kata ya mbumi wilayani kilosa
wanaadhiliwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na mifereji kuwa michache na
iliyopo kujaa tope pamoja na wananchi kutumia mifereji hiyo kutupa takataka
ndani ya mifereji hiyo.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi B Ally
Mdimu na kuongeza kwa kusema kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
wilayani kilosa kumekuwa na chemchem ya maji mengi yanayoweza kusababisha
athari katika makazi ya watu hivyo amewataka wananchi kuwa makini na matumizi mazuri ya misingi inayotumika kusafirishia
maji kwani amesema kuwa kuna baadhi ya wananchi wanatupa takataka katika
misingi hiyo
Aidha mtendaji wa kata ya Mbumi Rajabu Mhina amewataka
wananchi kuyajari mazingira yao kwa kuyafanyia usafi na kuacha tabia ya
kuitegemea serikari kwa kila kitu.
Nao wananchi wa kata hiyo ya Mbumi Sarehe Nasoro Hamisi na
Paskolina Mtinda wanawaomba wananchi wenzao kuyajali mazingira yanayowazunguka
na kuacha tabia ya kutupa takataka katika misingi hiyo inayopitisha maji
hayo.
No comments:
Post a Comment