BAADHI YA VIJANA AMBAO NI AWALI WALIKUWA WANACHAMA WA CHADEMA WAKIONYESHA KADI ZAO MPYA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM |
Vijana zaidi
ya 100 ambao ni wanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA wilaya
ya Ulanga mkoani Morogoro wamekihama
chama hicho na kujiunga na chama cha
mapinduzi (CCM).
MRATIBU WA WAZEE WA CHADEMA NDUGU ZIMANI NA KATIBU KATA WA CHAMA HICHO WILAYANI HUMO DEODATUS CHARLIES, WAKIKABIDHI BENDERA ZA CHAMA HICHO KWA UONGOZI WA CCM. |
Hatua hiyo
ya wanachama hao wa CHADEMA kujiunga na CCM imekuja kufauatia maendeleo
mbalimbali yanatekelezwa na mbunge wa jimbo hilo la Ulanga Mashariki Serina
Kombani, Kama vile ujenzi wa Barabara na ujenzi wa Soko.
Baadhi ya viongozi wa CCM na wale kutoka chama cha CHADEMA waliokiama chama hicho na kujiunga na CCM |
Uwajibikaji
wa viongozi wa serikali katika majukumu yao wilayani humo ni moja ya sababu
inayowafanya wanachama wa vyama vya
upinzani kurudi chama cha mapinduzi CCM.