Diwani wa kata ya masanze wilayani kilosa mkoani morogoro
Jonathani Kambikiye ameongoza harambee ya uchangiaji wa vifaa vya ujenzi wa
kanisa la Aglikana kijiji cha Dodoma Isanga kilichopo kwenye kata hiyo.
Harabee hiyo imefanyika hivi karibuni baada ya Ibada ya
jumapili ambayo imeongozwa na mchungaji Mwegalawa wa kanisa la Aglikana parishi
ya zombo na Area Dean wa dinari ya zombo.
Kambikiye ameongoza zoezi hilo la harambee ya upatikanaji wa vifaa vya
ujenzi ambapo waumini wa kanisa hilo la kijiji cha Dodoma Isanga na viongozi na
wadau mbalimbali wameweza kukamilisha vifaa vyote kwa ajili ya kuezekwa kanisa
hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1983 vimeweza kukamilika hivyo kuwa na uhakika
wa ujenzi huo wa nyumba ya Mungu.
Vifaa vilivyokuwa vikihitajika ni pamoja na bati 30 mbao 70
na misumari kilo 15 ambapo Diwani huyo amechangia bati tano na kilo nne za
misumari ili kuwapa nguvu waumini hao kwa ajili kukamilisha ujenzi wa kanisa
hilo.
Akizungumza baada ya
harambee hiyo Diwani huyo wa kata ya Masanze Jonathani Kambikiye amewashukuru
wote waliochangia vifaa hivyo ili kukamilisha ujenzi huo wa kanisa na kuwataka
wazee wa kanisa hilo kuhakikisha wanasimamia ipasavyo zoezi hilo la nyumba ya
Ibada.
No comments:
Post a Comment