Polisi mkoani morogoro inamshikilia Karume Kauzu Habibu Mkazi wa Riti kwa kujifanya daktari katika
haspitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro ambapo amekuwa akioneka maeneo
hayo huku akiwa mevalia mavazi ya udaktari.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi Renard Paulo amethibitishwa
kutokea kwa tukio hilo na amesema mtuhumiwa huyo baada ya kukaguliwa
amekutwa na vitambulisho vinne tofauti huku kingine kikionyesha anajiandaa
kurudia mtihani wa kidato cha nne, makazi yake yakiti RITI mkoani Morogoro na
huku kitambulisho chake kimoja kinaonyesha kuwa alikuwa anasoma Kigoma.
Daktari feki aliyevaa koti jeupe Karume Kauzu Habibu akiwa chini ya ulinzi |
Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji Francis Semwene amesema alipata taarifa toka kwa muuguzi wa zamu na kuweka mtego ulifanikisha kukamatwa kwa daktari huyo feki.
No comments:
Post a Comment