Chama cha mapinduzi CCM wilayani Kilosa mkoani Morogoro
kimesikitishwa na hali inayojitokeza katika hospital ya wilaya kwa baadhi ya
wauguzi wa afya kutoa lugha chafu kwa
wagonjwa mara wanapokwenda kupata matibabu hospitalin hapo.
Hayo yameelezwa na katibu
waccm wilaya ya Kilosa Dodo Sambu hivi karibuni wakati wa kikao na
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya
baada ya wazee hao kutoa malalamiko kuhusu wagonjwa kunyanyaswa na watoa huduma
hao .
Dodo ameeleza kuwa chama cha mapinduzi kimepokea kwa
masikitiko yanayotolowe na wananchi na wazee juu ya vitendo vya kutolewa
lugha chafu vinavotendwa na watoa huduma hospitalini
hapo.
Amesema kuwa watoa huduma hao wa afya wanapaswa kuhudumia
vizuri na kwa upendo wagonjwa mara
wanapofika kupata matibabu kwa kufuata maadili ya kazi zao.
Dodo ameongeza kuwa
malamiko ambayo yanayotolewa kwenye kuwahudumia wagonjwa hospitalini hapo
yanatendwa na watoa huduma hao ambao
wanasahau kuwa waliapa kuwahidumia
vizuri wagonjwa hivyo kufuatia hali hiyo chama cha mapinduzi wilaya
kinaiomba halmashauri ya wilaya kuwachukulia hatua wahudumu hao ikiwemo kupumzishwa kazi.
No comments:
Post a Comment