Mkuu wa
wilaya kilosa mkoani morogoro Elias Tarimo amewataka wahudumu wa sekta ya afya
wilayani humo kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata maadili ya kazi zao.
Ametoa kauli
hiyo hivi karibuni wakati wa kikao na wajumbe wa baraza la wazee wilaya, mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri wilaya,Viongozi wa vyama vya siasa na Baadhi ya
wataaramu wa aiadaza za Halmashauri ya wilaya kilosa.
Tarimo
ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na wazee wa
baraza hilo,ya kuwa wahudumu wa afya katika hospitali ya wilaya ,wanatabia ya
kuwatolea lugha chafu mara wanapofika kwa ajili ya kupata matibabu hospitalini
hapo.
Aidha amesema
kuwa wanapaswa kuhudumia wagonjwa kwa kauli nzuri na upendo kwa wagonjwa
wanahitaji kupokea na kupatiwa huduma kwa faraja si kuwatolea lugha
chafu,ambapo baadhi wamekuwa wakitoa malalamiko kila siku juu ya watoa huduma
hao wa sekta ya afya huwafokea na kuwanyanyasa wagonjwa.
Ameongeza
kwa kusema kuwa changamoto zinazovikabili vituo vya afya wilayani humo zikiwemo
dawa na watoa huduma,amesma serikali itaendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo
ikiwemo kutoa kipaumbele kwa wazee kwa kuandaliwa kadi za matibabu ili
wazitumie mara wanapokwenda kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment