Imeelezwa
kuwa licha ya Mwenge wa Uhuru kupita katika Tarafa ya Mikumi Wilayani Kilosa
Mkoani Morogoro na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi wa
maji ambapo mpaka sasa hayajaanza kutoka katika Tarafa hiyo.
mradi wa maji mikumi
Hayo
yameelezwa na baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Mikumi Shafii Makiwa na Gaudensia
Aloyce wakati wakizungumza na HABARIKWANZA julai mbili mwaka
huu.
Wananchi hao
wamesema kuwa tatizo la ukosefu wa maji katika Tarafa hiyo ni la muda mrefu
kwani tangu Mwenge wa Uhuru kuzindua mradi wa maji safi na salama hadi sasa
hakuna jitihada zinazofanyika ili kuhakikisha changamoto ya maji inatatulika
katika Tarafa hiyo hali inayosababisha maisha kuzidi kuwa magumu siku hadi
siku.
Kwa upande
wake Mbunge wa jimbo la Mikumi Abdusalama Amer maarufu kwa jina la Sasgas
wakati akizungumza na HABARIKWANZA amekiri kutokuwepo kwa maji katika Tarafa
hiyo na kuahidi maji yataanza kutoka mapema mwezi wa nane mwaka huu.
Mbunge wa jimbo la mikumi Abdulsalama Amer
Amer amesema
kuwa sababu ya kutokutoka kwa maji kwenye mradi huo ni kutokana na mkandarasi
kuishiwa fedha za kumalizia mradi wa maji kwa wakati lakini kwa sasa fedha
imepatikana kwani bajeti hiyo imeshapitishwa Bungeni Mjini Dodoma hivi
karibuni.
Aidha Mbunge
huyo amewatoa wasiwasi wananchi wa Tarafa ya Mikumi kwa kusema kuwa maji safi
na salama lazima yatoke katika maeneo hayo kwani atahakikisha anatatua
changamoto zote zinazowakabili hususani ya maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment