Mama mmoja anayefahamika
kwa jina la Mwamini Juma [20] mkazi wa mamoyo wilayani Kilosa mkoani Morogoro
anadaiwa kumtelekeza motto Selemani Salumu mwenye umri wa miaka mitatu (3) kwa
shangazi zake naye kwenda kwa wanaume.
Kwa majibu wa shangazi zake
Mwamini Juma ambaye ni mwasham Salumu na
Halka Salum wamesema kuwa motto wao huyo mwamini salumu ambaye ni motto wa kaka
yao anatabia ya kumtekeleza mtoto mara kwa mara na kwenda kwa wanaume wengine
huishi nao na mwisho wa siku naye huachwa.
Aidha wamesema kuwa mtoto Mwamini
Juma alipewa mimba akiwa na umri wa miaka 17 na kijana anayefahamika kwa jina
la Doto salumu mkazi wa mamoyo wilayani Kilosa mkoani Morogoro ambapo mwaka
2011 alimpa mimba mtoto waliongea juu ya matunzo ya mtoto na kukubaliana katika
malezi ya kumlea mtoto atakayezaliwa lakini kijana huyo hakufanya hivyo na
kuamua kutoroka majukumu ya kumtunza mwanaye.
Kwa upande wake mama wa mtoto
Selemani Salumu ambaye anasadikisha kumtelekeza mtoto wake mara kwa mara
amethibitisha kumtelekeza mtoto wake huyo na kwenda kwa wanaume na kusema kuwa
siku alipoondoka nyumbani kwa mara ya mwisho alielekea chanzuru ambapo huko alienda kwa Ally Mkubuge
akidai kuwa ni rafiki yake . Na kufafanua kuoa
anapotoroka huwa anaogopa kurudi nyumbani mapema kutokana na shangazi
zake kumpiga kwa kile anachokitenda cha kutoroka na kumuacha mtoto nyumbani.
No comments:
Post a Comment