Mtoto anayefahamika kwa
jina la Devota Dalule mwenye umri wa miaka saba (7) mkazi wa Dumila Wilayani Kilosa Mkoani
Morogoro amefungiwa ndani kwa muda wa
miaka saba na Mama yake mzazi anayetambulika kwa jina la Sarah Mazengo mwenye
umri wa miaka 39 mkazi wa Dumila Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kutokana na
mtoto huyo kuwa na ulemavu wa miguu .
Mtoto Devota Dalule akiwa hopspitali ya wilaya ya kilosa
Kwa mujibu wa Daktari
Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kilosa Shedrack Mponzi amesema mtoto huyo amefika hospitalini hapo usiku wa kuamkia julai 12 mwaka huu akiwa tatizo la Utapiamlo na kusema kuwa hali yake
bado haijatengemaa na leo hii amepewa rufaa ya kwenda hospitali ya mkoa wa
Morogoro kwa matibabu zaidi.
Kwa upande wake Afisa
Ustawi wa Jamii wilayani Kilosa Saidi Kataluma amesema kuwa matatizo haya ya
utesaji na unyanyasaji wa watoto kwa wilaya ya Kilosa tatizo hilo ni la pili la
kwanza limetokea julai 3 mwaka huu lililomuhusisha mtoto aliyefahamika kwa jina
la Selemani Salumu mwenye umri wa miaka mitatu (3) ambaye ametelekezwa na mama
yake mzazi Mwamini Juma mwenye umri wa miaka 20 kutokana na mtoto huyo kuwa na
kichwa kikubwa. Na tukio la pili ni hili la mtoto Devota Dalule ambapo
inasemekana mtoto huyo amewekwa ndani kwa kipindi chote cha miaka saba na
kutopata huduma muhimu kama chakula pamoja na mavazi na inasemekana kuwa mama
huyo humficha mtoto huyo uvunguni ili asionekane kwa watu kutokana mtoto huyo
kuwa na ulemavu.
muuguzi wa hospitali ya wilaya kilosa akimuhudumia mtoto Devota Dalule
Kataluma amewataka wananchi
kuendelea kufichuwa maovu yote yanayotendeka katika jamii kwa ajili ya
kutokomeza matatizo hayo ya ukatili dhidi ya watoto wadogo.
Kwa upande wao wananchi wa
Wilayani Kilosa Lameck Mkude na Jane
Amandus wamesema kuwa vitendo hivi vinahathiri sana ukuaji wa mtoto na
wameviomba vyombo vya sheria pamoja na wananchi kusimamia mambo haya kwa ajili
ya kuweza kuyatokomeza na wameongeza kuwa mtoto hata kama atakuwa na ulemavu
ana haki ya kuishi kama mtoto asiye na ulemavu.
No comments:
Post a Comment