Shirika la usaidizi wa
kisheria mkoano morogoro Paralegal limeendesha mdahalo wa kupinga ukatili wa
kijinsia julai 5 mwaka huu wilayani kilosa mkoani mkoani morogoro.
Akizungumza katika mdahalo
huo Meneja wa shirika hilo mkoani morogoro Flora Masoy amesema kuwa wanatoa
mafunzo hayo kwa wananchi ili waweze
kujitambua na kutokomeza vitendo hivyo
vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vitendo vya ukatili hufanyiwa akina
mama pamoja na watoto.
Wajumbe wakiwa kwenye mdahalo
Wakizungumza katika mdahalo huo baadhi ya wajumbe katika mdahalo huo Baby Mussa na Stella Venus wamesema kuwa wanalishukuru shirika la Paraleg kwa kutambua maovu yaliyoko kwenye jamii na kuamua kuhamasisha wananchi kuachana na ukatili wa kijinsia kwa kutumia midahalo hiyo na kuongeza kuwa wanaomba katika mchakato wa kuipata katiba mpya wajumbe waliangalie swala la usawa kati ya mwanamke na mwanaume katika jamii .
Aidha wamesema kuwa waliyoyapata
katika mdahalo huo kwenda kuyatendea kazi katika jamii zao wanapotoka na
kuhahakikisha kila mtu anapata haki yake kwa kusema kuwa kwa wilaya ya kilosa
wanaume wanaume hutelekeza familia kwa mwanamke, mwanamke kuamrishwa kutozaa na
mwanamke kukosa haki yake ya kimsingi katika ugawaji wa mirathi na kusema kuwa
watasimama imara katika kupatikana kwa haki kwa kila mtu.
Mmoja wa wajumbe wakiwa kwenye mdahalo wakijadiliana kuhusu ukatili wa kijinsia
Wajumbe wakiwa kwenye vikundi kujadiliana kuhusiana na mada ya ukatili wa kijinsia
Mmoja wa wajumbe wakiwa kwenye mdahalo wakijadiliana kuhusu ukatili wa kijinsia
Wajumbe wakiwa kwenye vikundi kujadiliana kuhusiana na mada ya ukatili wa kijinsia
No comments:
Post a Comment