Thursday, September 28, 2017

UVCCM YAFANYA UCHAGUZI KUWAPATA VIONGOZI WAPYA WILAYANI KILOSA

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Kilosa Septemba 25 mwaka huu wamefanya uchaguzi wa Viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Vijana kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Uchaguzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa MT lodge uliopo Mjini Kilosa na kuudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa chama hicho wa Wilaya na ambapo ndugu Salehe  Nasibu Mhando amefanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya kwa kupata ushindi wa jumla ya kura 311 na kuwapita wapinzani wenzake wawili ambao ni Malko Madenge aliepata kura 65, Catherine Mtugo aliepata kura 134 ambapo idadi ya kura zote zilizopigwa ikiwa ni 524 huku zilizoharibika ni kura 14.

Akizungumza baada ya kuapishwa mwenyekiti huyo mpya Salehe Nasibu Mhando amesema anawashukuru wajumbe wote waliojitokeza kumpigia kura na kuahidi kuwa atahakikisha kutenga ofisi za Vijana katika kila eneo kuutumikia umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi kwa kutumia baraza la wilaya kwa kushirikiana na kamati ya utekelezaji ili kusaidia umoja huo kuwa na idadi kubwa ya vijana kwenye chama tawala.

Naye Mwenyekiti aliemaliza muda wake Michael Mkolokoti amemshauri Mwenyekiti Huyo mpya kuhakikisha anawasaidia vijana kwa kuwaondoa katika hali ya kutumika vibaya bila manufaa hasa kipindi cha uchaguzi.

Friday, August 18, 2017

WAFANYAKAZI WATAKIWA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI ILI WAWEZE KUNUFAIKA NACHO

Chama cha Wafanyakazi Wilayani Kilosa kimewataka Wafanyakazi kutoka kwenye Taasisi na Mashirika mbalimbali kujiunga na chama hicho ili kiwasaidie pindi wanapodhurumiwa haki zao.

Hayo yamesemwa na Katibu Msaidizi kanda ya Mashariki wa Chama cha Wafanyakazi Wilaya ya Kilosa  Gerald Edgar Tayari alipokua akitatua moja ya mgogoro wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Mbeula Security Guard Limited ambao hawakupata malipo yao.

Wakizungumzia mgogoro huo baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo Chacha Paulo, Maiko Msagati, Tausi Ally na Kaniki Kusekwa wamesea kuwa hawajapata malipo yao tangu walipoanza kufanya tarehe 12/7/2017 hadi agost 18 mwaka huu na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo kutoweka eneo la kazi pasipo na taarifa maalum kwa Wafanyakazi wake na wanapojaribu kuwasiliana nae kwa njia ya simu hapatikaniki.

Aidha kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo Mpemba Erasto amesema kuwa hana taarifa kamili yakuondoka kwa bosi wake kwani aliondoka huku akidai kuwa anafuata vifaa vya ulinzi lakini tangu alivyoondoka hadi sasa hakurejea kazini.

Thursday, August 3, 2017

WAMAMA WATAKIWA KUWAPA WATOTO WAO LISHE BORA


WANANCHI WILAYANI KILOSA WAMETAKIWA KUZINGATIA UMUHIMU WA LISHE BORA NA TARATIBU SAHIHI ZA ULISHAJI WATOTO WACHANGA NA WADOGO ILI KUKABILIANA NA TATIZO LA UTAPIAMLO.

HAYO YAMEELEZWA AGOST 2 NA KAIMU MGANGA MKUU WA WILAYA THOMASI KIBULA KWA NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI AMBAYO IMEANZA AGOST 1 NA ITAFIKA TAMATI AGOST 7 MWAKA HUU.

KIBULA AMESEMA KAULI MBIU YA MWAKA HUU KWENYE MAADHIMISHO HAYO NI ''SOTE KA PAMOJA TUENDELEZE UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA " MAADHIMISHO HAYO YAMEBEBA UJUMBE UJUMBEAALUMU UNAOLENGA KUHAMASISHA NA KUONGEZA UELEWA WA JAMII KUHUSU IMUHIMU WA LISHE BORA KWA WATOTO NA TARATIBU SAHIHI ZA UZALISHAJI WATOTO WACHANGA NA WADOGO ILI KUKABILIANA NA TATIZO LA UTAPIAMLO.

AMEONGEZA KWA KUSEMA MAADHIMISHO HAYO YANALENGO LA KUSISITIZA UMUHIMU WA KULINDA, KUIMARISHA NA KUENDELEZA UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA ILI WATOTO WAKUE KATIKA AFYA NJEMA.

TANZANIA HUUNGANA NA NCHI NYINGINE DUNIANI KUADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA.