Friday, September 19, 2014

MAHAFARI YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA MSINGI KICHANGANI NA MKWATANI ZILIZOPO WILAYANI KILOSA

Wahitimu wa darasa la saba katika shule mbili za  msingi za mkwatani na kichangani zilizopo wilayani kilosa mkoani morogoro wametakiwa kuwa makini kwa kipindi hiki ambacho wamehitimu elimu ya msingi wakiwa wanasubili  wakiwa nyumbani kwa kungojea matokeo yao.

                             Waitimu wa darasa la saba wa shule zote mbili mkwatani na kichangani
Hayo yamesemwa na aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo  Faresi Makene alipokuwa akiwapa wosia wahitimu hao wa darasa la saba September 19 mwaka huu katika viwanja vya shule ya msingi kichangani ambapo katika shule ya msingi kichangani waliohitimu ni 72 na katika shule ya msingi mkwatani wanafunzi waliohitimu ni 22.
Mwalimu mkuu wa shule ya mkwatani aliyesimama akifuatiwa na mgeni Rasmi akifuatiwa na mwenyekiti wa shule ya msingi kichangani Swedy Sawasawa na wa mwisho ni  Mwalimu wa shule ya msingi kichangani Saidy Mkalimoto
                  Baadhi ya wazazi wakiwa wanawashuhudia watoto wao wakihitimu elimu ya msingi
                                      Wanafunzi wa darasa la sita wakiwa wanacheza muziki


Katika mahafari hayo pia Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mkwatani  Sophia Mkwemba amewataka wazazi na viongozi wa vijiji kuwapokea watoto hao huko majumbani na kuwa nao makini kwa kuedelea 



wanafunzi na wazazi waliokusanyika kuwaaga wahitimu wa darasa la saba katika viwanja vya shule ya msingi kichangani.
kuwapa na kuwafunza maadili yaliyo mema ili kuwaandaa na maisha ya baadae na kuwataka wazazi 
kujiandaa mapema pindi matokeo yanapotoka ili wawasomeshe vizuri watoto bila matatizo.

                                           Mzazi akifurahi na mwanaye mara baada ya sherehe
   kikundi cha ngoma cha wanafunzi wa darasa la nne wakitumbuiza katika sherehe hiyo ya mahafari ya darasa la saba 2014

Wednesday, September 3, 2014

WANANCHI WA WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO WACHOSHWA NA UONGOZI ULIOPO MADARAKANI KWA KUSHINDWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI



Wanakijiji wa ulaya mbuyuni  kata ya ulaya wilayani kilosa mkoani morogoro wameilalamikia serikali ya kijiji na Tarafa kwa kutowatatulia mgogoro wao uliopo unaowahusu wafugaji kuwavamia katika maeneo yao ya kilimo.
                                                    Mifugo ikiwa inashambulia zao la mbaazi

Wakitoa malalamiko yao kwa Jazba September 2 mwaka huu kwenye mkutano wa kijiji ulioitishwa na Afisa Tarafa Baadhi ya wakulima katika kijiji hicho cha ulaya mbuyuni Twist Twaha Kilabeba,Steven Mzuma na Omary Mbwana alimaarufu kwa jina la [Gulamali] wamesema kuwa wamechoshwa na uongozi uliopo madarakani hasa uongozi wa kijiji kwani umeonyesha dalili za kushindwa kutatua mgogoro wao kwa muda mrefu hali ambayo inawafanya kukosa amani katika mashamba yao na uhai wao kiujumla kwani wafugaji hao wa jamii ya kimasai huwatishia wakulima hao.
                    Baadhi ya mazao aina ya mbaazi ikiwa imeharibiwa na mifugo aina ya ng'ombe

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo amesema kuwa wafugaji waliokuwa maeneo ya wafugaji wanapaswa kuondoka haraka sana kwani kisheria watakamatwa na kufunguliwa mashtaka na kuongeza kuwa amewaagiza maafisa tarafa kwa ajili ya utekelezaji wa kuwaondoa wafigaji hao na ameongeza kuwa wananchi hawapaswi kutoa maeneo yao kwa ajili ya kulisha mifugo na badala yake wakibainika watakamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani na kwa upande wa viongozi kama wakibainika kuwapokea wafugaji kinyemela watawajibishwa kinidhamu kufunguliwa mashtaka mahakamani pamoja na kuwaondoa madarakani.
Aidha Afisa tarafa wa Tarafa ya Ulaya Raphael Mvulungu amewaomba wananchi kutuliza jazba zao na kuwaomba kutoa ushilikiano wao kwa ajili ya kuwaondoa wafugaji hao wa jamii ya kimasai na kusema kuwa wafugaji hao hawawezi kuleta ubishi wa kuondoka ila kutakuwa na watu watakao kuwa wanawakingia kifua na kusema kuwa kuna baadhi ya wananchi wananufaika na wafugaji hao na baadhi yao walimwambia wafugaji hao wasiondoke walipoambiwa kuna mchakato wa kuwaondoa.
Aidha Mvulungu ameongeza kuwa katika zoezi la kuwaondoa wafugaji hao ataanza na wale ambao wametoa maeneo yao kwa ajili ya kuwapa wafugaji hao kwa ajili ya kujenga mazizi na wale wakulima ambao wanatoa maeneo yao kwa ajili ya kulishia mifugo na kuongeza msisitizo kuwa atahakikisha wafugaji hao wanaondoka katika kijiji hicho kikubwa amewaomba ushilikiano wananchi kwa ajili ya kuwaondoa wafugaji hao.