Friday, August 18, 2017

WAFANYAKAZI WATAKIWA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI ILI WAWEZE KUNUFAIKA NACHO

Chama cha Wafanyakazi Wilayani Kilosa kimewataka Wafanyakazi kutoka kwenye Taasisi na Mashirika mbalimbali kujiunga na chama hicho ili kiwasaidie pindi wanapodhurumiwa haki zao.

Hayo yamesemwa na Katibu Msaidizi kanda ya Mashariki wa Chama cha Wafanyakazi Wilaya ya Kilosa  Gerald Edgar Tayari alipokua akitatua moja ya mgogoro wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Mbeula Security Guard Limited ambao hawakupata malipo yao.

Wakizungumzia mgogoro huo baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo Chacha Paulo, Maiko Msagati, Tausi Ally na Kaniki Kusekwa wamesea kuwa hawajapata malipo yao tangu walipoanza kufanya tarehe 12/7/2017 hadi agost 18 mwaka huu na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo kutoweka eneo la kazi pasipo na taarifa maalum kwa Wafanyakazi wake na wanapojaribu kuwasiliana nae kwa njia ya simu hapatikaniki.

Aidha kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo Mpemba Erasto amesema kuwa hana taarifa kamili yakuondoka kwa bosi wake kwani aliondoka huku akidai kuwa anafuata vifaa vya ulinzi lakini tangu alivyoondoka hadi sasa hakurejea kazini.

No comments:

Post a Comment